Rais Samia: Ondoeni watumishi wanaobabaisha

0
42

Rais Samia Suluhu Hassan amesema watu wanaotengeneza fitina ndani ya Serikali kwa sababu watu wao wamekosa tenda mbalimbali za Serikali wanakwamisha miradi inayofanyika na maendeleo kwa ujumla.

Akizungumza leo Februari 14, 2023 wakati akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa miradi mahsusi ya umeme Ikulu jijini Dar es Salaam, ameiagiza mamlaka na taasisi za Serikali kupima kila kinachoripotiwa kwao ili kuepusha kukwama kwa miradi.

“Uteuzi wa wakandarasi hawa unafanywa kwa umakini mkubwa sana. Natambua kuna wenzetu wengi ambao kila mtu alikuwa na mkandarasi wake mkononi na alipenda apate, na kwa sababu hakupata fitina ni nyingi [..] kwa matakwa yao binafsi,” amesema.

Rais Samia kununua kila goli la Simba na Yanga kwa TZS milioni 5

Aidha, ametoa wito kwa wakuu wa mashirika mbalimbali wasiogope kufanya mabadiliko ya watendaji endapo hawatoendana na kasi ya Serikali na kuwataka watumishi kuwajibika na kufanya kazi kwa ufanisi.

“Kama mnabadilishwa hautaki kubadilishwa onesha unaweza, unafanya kazi, unaonesha ufanisi hutoondolewa. Lakini kama unababaisha, huwezi utaondoka,” amesisitiza.

Katika hotuba yake Rais Samia amesema pamoja na mafanikio makubwa katika kupeleka umeme vijijini, bado kuna kazi ya kufanya kwa kuwa kati ya vitongoji 64,760 vilivyopo nchini ni vitongoji 28,424 pekee ndivyo vimepata umeme, sawa na asilimia 43.9.

Send this to a friend