Rais Samia: Serikali haitakubali kusalitiwa

0
40

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Makatibu Mahsusi, Watunza Kumbukumbu pamoja na maafisa utumishi kutunza siri za Serikali wanazozijua katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Ametoa agizo hilo leo wakati akifungua Mkutano wa Tisa wa Kitaaluma wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) na kuongeza kuwa suala la utunzaji wa siri linasaidia kuepuka madhara yanayoweza kuwapata watu binafsi, taasisi, serikali na usalama wa Taifa.

“…mkiamua kusaliti tutashikana huko mbele. Hatutakubali kusalitiwa,” ametahadharisha Rais Samia.

Pia, amesema weledi, uaminifu, uadilifu na uzalendo ndiyo njia pekee itakayowafanya Makatibu Mahsusi kuaminiwa, kutegemewa na kuwawezesha kusonga mbele katika majukumu yao.

Katika hatua nyingine, Rais Samia ameridhia Chuo cha Utumishi wa Umma Tabora kuwa maalum kwa ajili ya mafunzo ya uhazili kwa ngazi zote ili kuzalisha Makatibu Mahsusi ambao watakwenda kutumika katika Taasisi za Serikali.

Halikadhalika, Rais Samia amesema Serikali inaendelea kuimarisha miundo mbalimbali ya kada za kiutumishi, na maslahi ya watumishi wa umma kwa ujumla.

Send this to a friend