Rais Samia: Serikali haitofanya biashara bali sekta binafsi

0
41

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali haitafanya biashara bali inatengenezea mazingira mazuri kwa ajili ya sekta binafsi ya ndani ya Tanzania au nje.

Ameyasema hayo leo wakati akishiriki kongamano la wafanyabiashara wa Oman na Tanzania pamoja na kushuhudia utiaji saini makubaliano ya ushirikiano wa pamoja katika sekta mbalimbali nchini Oman.

“Sekta binafsi iendeshe uchumi, Serikali ikiendelea kuboresha mazingira ya biashara na ushirikiano. Serikali tunatengeneza mazingira mazuri kwa sekta binafsi ya ndani au nje kufanya biashara nchini,” amesema Rais Samia.
 
Aidha, ametaja kuwa ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na Oman umechagizwa na amani iliyopo Tanzania pamoja na utawala bora.
 
Hata hivyo ameeleza kwamba kwa kushirikiana na Oman, serikali itatatua changamoto nyingi za kiuchumi ikiwemo ukosefu wa vyombo vya usafiri hususani usafiri wa baharini.
 
 
 
 
 

Send this to a friend