Rais Samia: Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili

0
52

Kufuatia mauaji ya kikatili yaliyotokea kwa aliyekuwa Mjumbe wa Sekretariati ya CHADEMA, Ally Mohammed Kibao, Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza vyombo vya uchunguzi kutoa taarifa za kina juu ya tukio hilo.

Mwili wa Kibao umeokotwa siku ya jana usiku katika eneo la Ununio Dar es Salaam ukiwa na majeraha ya kupigwa huku akiwa amemwagiwa tindikali usoni na watu wasiojulikana ambao wanadaiwa walimchukua akiwa katika basi la TASHRIF wakati akitokea Dar es Salaam kuelekea Tanga.

“Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.

Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi,” ameeleza.

Aidha Rais Samia amesisitiza kuwa Serikali anayoiongoza ya awamu ya sita, haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hiyo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Send this to a friend