Rais Samia: Sifurahii kubadili viongozi, inachukua muda kuwajenga

0
23

Rais Samia Suluhu Hassan amesema hulazimika kuwabadili viongozi mara kwa mara ili kuepusha madhara zaidi kwa Serikali na wananchi ambayo yangeweza kutokea.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa faragha wa mawaziri, naibu mawaziri, makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu katika Kituo cha Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha, amesema hafurahishwi kufanya hivyo kwa kuwa viongozi hufanya kazi kwa hofu wakihofia teuzi zao kutenguliwa.

“Kiongozi anapoondoshwa kazini ni fedheha kwa familia yake, watoto na vijana ambao walikuwa wanamuona kama mtu wa mfano au role model, na mimi si lengo langu kubadilisha viongozi mara kwa mara kwa kuwa huchukua muda mrefu kuwajenga,” amesema.

Waziri Nape: Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi Tanzania

Aidha, amesema viongozi wazoefu ndiyo wanafanya viongozi wapya waige mienendo yao wakijua kwamba kuwa na migogoro, kutofuata sheria na taratibu ni jambo la kawaida Serikalini.

Katika hotuba yake pia amewata viongozi kuepuka kauli zinazowafanya wawekezaji kutilia shaka dhamira ya Serikali pamoja na kuepuka lugha isiyofaa inayoweza kusambaa katika mitandao ya kijamii.

“Tunapokwenda huko nje, tunakwenda na lugha nzuri, tumefanya hiki, tumerekebisha hiki. Tunawaita njooni muwekeze kwetu wanakuja kwa wingi, wanapofika ofsini maneno wanayoyapata yanawarudhisha nyuma,” ameeleza.

Send this to a friend