Rais Samia: Siwezi kutia mkono suala la Wabunge 19

0
47

Rais Samia Suluhu amesema Serikali imefanya ubunifu wa kuhakikisha taifa la Tanzania linaungana na kuwa na umoja kwa kuvifanya vyama vya siasa kupitia taasisi zake kukaaa na kueleza changamoto zillizopo.

Akizungumza katika kongamano la Siku ya Wanawake Duniani Machi 08, 2023 iliyoandaliwa na Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) mkoani Kilimanjaro, Rais Samia amesema si rahisi watu kuukubali utamaduni mpya wa maridhiano mpaka pale watakapoona matunda yake.

  Rais Samia akemea viongozi kusengenyana na kudharau wananchi

“Hakuna mwanadamu kaumbwa anapenda ugomvi tu vurugu, fujo hakuna, kila mwanadamu anapenda amani ya roho yake, kwa hiyo twendeni tujenge amani za nyoyo zetu.” amesema

Aidha, amesema taifa linapaswa kukuza siasa za kistaarabu na maelewano na si kushambuliana kwa kuwa usalama na amani vitakapopotea katika nchi wanaoathirika ni wanawake na watoto.

Kuhusu suala la kesi ya wabunge 19 (Halima Mdee na wenzake) ambayo ameombwa kulitazama kwa ukaribu, ameeleza kuwa hawezi kutia mkono suala hilo kwa kuwa kesi yao ipo mahakamani.

 

“Hilo la mwisho kwa jina hilo mliloliita [COVID19], wote wawili waliowasilisha malalamiko wamesema hapa ‘Japo kesi ipo Mahakamani lakini Mama..’, naomba niwaambie tuachie mkondo ule uendelee tutazame mbele yanayokuja, sio rahisi hata kama Mimi ni Rais kutia mkono huko, tuache mkondo uendelee tutazama yanayokuja,

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amemshukuru Rais Samia kwa kulinda kwa kiasi kikubwa makubaliano na kuyapa nafasi mazungumzo na maridhiano kwa hatua zote kupitia vyama vvikubwa vya siasa.

Send this to a friend