Rais Samia: Tamasha la Kizimkazi linachochea miradi ya maendeleo
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tamasha la Kizimkazi limeendelea kujipambanua kuwa la kimaendeleo kwa kuchochea utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye manufaa makubwa kwa wananchi.
Ameyasema hayo leo wakati akifungua Skuli ya Maandalizi Tasani iliyoko Makunduchi ambapo amesisitiza kuwa njia bora ya kuwalinda watoto ni kuhakikisha wanapata fursa ya kusoma.
Aidha, amesema Serikali ina dhamira ya kuhakikisha watoto wote nchini wanapata malezi bora ikiwemo maandalizi mazuri yatakayowapa msingi mzuri wa mafanikio shuleni na maisha yao kwa ujumla.
Katika hafla ya kuhitimisha mafunzo na kugawa vyeti kwa washiriki wa mafunzo ya ujasiriamali, Rais Samia amewataka vijana kuchangamkia fursa za kupata mafunzo na ujuzi mbalimbali ili waweze kujikwamua kiuchumi.