Rais Samia: Tanzania bado ipo uchumi wa kati

0
37

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania haijashuka kutoka uchumi wa kati bali kilichorudi nyuma ni kasi ukuaji wa uchumi ndani kulikochangiwa kwa kiasi kikubwa na janga la UVIKO19.

Ameeleza kuwa awali uchumi wa Tanzania ulikua kwa asilimia 6.8, 6.9 mpaka asilimia 7,  yalipokuja maradhi ya UVIKO19 ulimwengu ulijifungia ukaacha kuzalisha na ndipo uchumi ukashuka mpaka kufikia kasi ya ukuaji ya asilimia 4.

“Uchumi ulishuka kwa factor [sababu] za nje, lakini ndani tuliendelea kufanya kazi ukuaji wetu ukawa 4% kutoka 6.8%, hii haijatutoa kwenye uchumi wa kati kwa sababu vigezo vyao kule ni tofauti, tunategemea labda 2025 tunaweza tukarudi kule tulipokuwa 6.8%,” amesema Rais Samia.

Rais ameongeza kuwa Tanzania iko katika nafasi nzuri ya ukuaji wa uchumi ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki pamoja na  Kusini mwa Afrika.

Send this to a friend