Rais Samia: Tanzania haiongozwi na utashi wa mataifa ya nje

0
21

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ni moja tu duniani ambayo ni taifa huru lililojengwa katika misingi ya amani, upendo na mshikamano na linaloongozwa kwa misingi ya Katiba na Sheria zilizotungwa na Bunge na sio utashi wa mataifa ya nje.

Amesema hayo wakati akifungua mkutano wa wadau wa siasa unaojadili hali ya demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini Tanzania, unaofanyika Jijini Dodoma.

Ametumia jukwaa hilo kutahadharisha kuwa siasa za maneno yasiyo na staha, kusema uongo, lugha za dhihaka, maneno ya kashfa, kuchochea watu wasishiriki katika shughuli za Maendeleo, kutotii sheria, uchonganishi baina ya wananchi hazina tija yoyote bali ni ukiukwaji wa kanuni za ushindani.

“Demokrasia ni kuheshimu sheria, unapoheshimu sheria ndipo demokrasia inapokua, lakini pia ndipo inapoleta heshima, heshima ya mtu inakuja kwa kuheshimu sheria za nchi, unapovunja sheria za nchi heshima yako haitaheshimiwa, Serikali haitakuheshimu lakini lazima ujue kwamba unapotumia uhuru wako mwisho wa uhuru wako huanza heshima ya mtu mwingine,” amesema hayo akijibu ombi la Zitto Kabwe kuhusu kuachiwa huru Freeman Mbowe.

Rais amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa pamoja na Vyama vya Siasa kukaa na kujadiliana katika Mkutano huo namna bora ya kufanya shughuli zao za mikutano ya kisiasa bila kuvunja sheria za nchini.

Send this to a friend