Rais Samia: Tumeboresha sera na sheria kukuza biashara na uwekezaji nchini

0
43

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imefanya maboresha mengi ya kisera, kisheria na kanuni ili kuhakikisha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini yanaendelea kuwa bora zaidi.

Rais Samia ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi waliofika kwenye mkutano wa hadhara mara baada ya kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa kiwanda cha vioo cha Sapphire Float Glas kilichopo Mkuranga mkoani Pwani.

“Mwaka jana 2022 tulitunga sheria mpya ya uwekezaji Tanzania ambapo kwa kiasi kikubwa imeweka mazingira bora ya uwekezaji na kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo utoaji wa vivutio kwa wawekezaji wa kimkakati kama huyu wa kiwanda hiki cha glass,” amesema.

Serikali kufanya utafiti kubaini kiasi cha dhahabu kilichopo nchini

Rais amesema kwa takwimu za Kituo cha Uwekezaji (TIC), mpaka Septemba mwaka huu kituo kimesajili jumla ya miradi 417 katika sekta ya viwanda kati ya Januari 21 na Septemba 15 yenye thamani ya TZS trilioni 12 ikiwa ni wastani wa dola za Marekani milioni 12 kwa kila mradi.

Aidha, amesema asilimia 75 ya bidhaa zitakazozalishwa katika kiwanda hicho zitauzwa nje ya nchi na hivyo kuleta fedha za kigeni nchini pamoja na kutoa ajira 1,650 pindi kitakapokamilika katika awamu ya kwanza.

Mbali na hayo, amesema Tanzania inaendelea kuboresha mahusiano mazuri na nchi za kigeni na mpaka sasa umeleta manufaa makubwa akitolea mfano wa nchi ya China ambayo mahusiano baina ya Tanzania na nchi hiyo yamekuwa ya kimkakati.

Send this to a friend