Rais Samia: Tunaendelea kutekeleza mazuri tuliyoyaanzisha awamu ya tano

0
42

 

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kazi zinazoendelea kufanyika ni mwendelezo wa yale mazuri waliyoyaanzisha katika awamu ya tano akiwa na Hayati John Pombe Magufuli.

Ameyasema hayo katika sherehe za maadhimisho ya miaka miwili ya uongozi wake yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam Machi 19, 2023.

“Mpaka leo hakuna kilichosimama tumeendelea kuyatekeleza tuliyoyaanza kwenye awamu ya tano na kuleta mapya ambayo ubunifu unatuongoza twende nayo mbele kwa mbele,” amesema.

Sherehe hizo zilizoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kutoka Chama Cha Mapinduzi zimehudhuriwa na  viongozi na wanachama wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) akiwemo Kaimu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Sharifa Suleiman, Devotha Minja na Susan Lyimo.

Aidha, Rais Samia ameahidi kuendelea kutekeleza yale yote ambayo yanayawaumiza wanawake na kuwakosesha huduma mbalimbali nchini ikiwemo kujenga shule za sayansi kwa kila mkoa pamoja na Vyuo vya Elimu Ufundi (VETA) kwa kila Wilaya.

“Lengo ni kuwafundisha vijana wetu teknolojia mbalimbali ili wawe wabunifu walete maendeleo Tanzania.” ameeleza

Send this to a friend