Rais Samia: Tunaimarisha mahakama ili haki ipatikane

0
17

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka majaji kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia misingi ya kutoa haki kwa kila mmoja bila upendeleo kama ambavyo wameaminiwa.

Akizungumza katika uwaapisho wa viongozi wateule jijini Dar es Salaam, amesema jinsi dunia inavyobadilika kiuchumi na kisiasa ndivyo Tanzania inapaswa kubadilika, na mabadiliko hayo hayalengi nguzo moja ya Serikali pekee bali mahakama na bunge pia.

“Ni imani yetu kuwa mlioteuliwa leo mtakwenda kufanya kazi kwa jitihada zenu zote katika Mahakama Kuu ili yale tunayoyatarajia yaonekane, mabadiliko tunayoyazungumza basi tuyaone ndani ya mahakama. Wakati Serikali inajitahidi kuimarisha mahakama na watendaji ndani ya mahakama tunaomba muongeze nguvu ili mwende mfanye vizuri,” amesema.

Rais Samia: Tumeruhusu mikutano vyama vikue, si kutukana na kuvunja sheria

Aidha, amesema madhumuni ya Serikali ni kuimarisha mahakama ili kuondoa mlundikano wa kesi na kuongeza ufanisi mahakamani, na moja ya hatua ambayo Serikali imechukua ni kuongeza idadi ya majaji ili kusaidia kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo.

Mbali na hayo, katika hotuba yake amewataka viongozi kwa ujumla kujiepusha kuondolewa katika nafasi zao Serikali kwa kutekeleza vyema majukumu yao ya kazi.

Send this to a friend