Rais Samia: Tusikubali kugawanywa kwa sababu za kisiasa

0
1

Rais Samia Suluhu Hassan amewasihi Watanzania kuwakataa wale wote wanaotaka kuligawa Taifa kwa sababu za kisiasa au tofauti za kiitikadi kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Ameyasema hayo katika kilele cha Tamasha la Tatu la Utamaduni la Kitaifa lililofanyika katika Uwanja wa Majimaji Songea, mkoani Ruvuma ambapo amewasisitiza Watanzania kutanguliza maslahi ya nchi kabla ya kutanguliza maslahi binafsi, pamoja na kutunza maadili na utamaduni wa Kitanzania.

“Niwatake Watanzania kutanguliza maslahi ya nchi kabla ya maslahi binafsi, tuwakatae wote wanaotaka kutugawa kwa sababu za kisiasa au tofauti za kiitikadi, Watanzania ni wamoja, Tanzania ni moja, sisi ni mtu mmoja,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amesema Serikali imejipanga kufungua vituo 100 vya lugha ya Kiswahili kote duniani kwa kushirikiana na Watanzania waishio nje ya nchi na kuwahimiza Watanzania waishio nje ya nchi kuchangamkia fursa hizo ambazo zitafungua milango ya kiuchumi na kujiingizia kipato.

Mbali na hayo, ameiagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Waziri Damas Ndumbaro kuhakikisha kuwa ushiriki wa Tanzania katika uandaaji wa michuano ya AFCON 2027unakuwa na manufaa kwa Watanzania, na kuhakikisha Tanzania inatengeneza alama Afrika na kidunia.

Send this to a friend