Rais Samia: Tusipochangia huduma za matibabu, huduma zitarudi nyuma

0
46

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wananchi kuchangia gharama za matibabu kwa kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anakuwa na bima ya afya ili kuiwezesha Serikali kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.

Akizungumza leo katika ufunguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mjini Magharibi (Lumumba), Zanzibar, amesema Serikali kubeba mzigo wote si rahisi hivyo wananchi wasipochangia, huduma za afya zitarudi nyuma na juhudi za Serikali katika kuboresha sekta hiyo zitakwenda bure.

“Pamoja na kwamba moja katika shabaha za mapinduzi ni kufanya matibabu yawe bure kwa wananchi lakini sasa ni miaka 60 tumekwenda mbele mno kuliko kule tulikokuwa. Hakukuwa na mwananchi mwenye uwezo wa kuwa na bima ya afya na ndiyo maana tukasema matibabu bure. Lakini tulipofika ili tuweze kutoa huduma endelevu, suala la bima ya afya haliepukiki,” amesema.

Rais Samia: Baadhi ya wahitimu vyuo hawawezi kufanya kazi wakiajiriwa

Aidha, amesema hospitali hiyo ya kisasa iliyofunguliwa Zanzibar ina vifaa vya kisasa vya TEHAMA na vifaa tiba ambavyo vinapatikana katika hospitali nyingine duniani, hivyo wananchi watapata huduma hizo ndani ya nchi badala ya kuzifuata nje ya nchi.

“Ni vifaa vile vile vinavyotumika kule ndivyo vinavyotumika hapa, hata upelekwe wapi vifaa vitakavyotumika ni hivi hapa,” ameeleza Rais huku akiwataka watumishi kuchapa kazi na kutoa huduma zinazoendana na majengo hayo.

Send this to a friend