Rais Samia: Tutaanza kutekeleza miradi kwa fedha za ndani

0
52

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali ya Awamu ya Sita inaanza mkakati mpya wa kutekeleza miradi ya kimkakati kwa kutumia fedha za ndani kabla ya kuhusisha washirika wa maendeleo, ili kuongeza kasi ya utekelezaji na kupunguza ucheleweshaji unaotokana na taratibu ndefu za nje.

Akizungumza leo  Novemba 18, 2025 wakati wa hafla ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha miradi ya maendeleo nchini inatekelezwa kwa wakati, huku serikali ikiweka mbele maslahi ya wananchi.

“Muhula wa pili wa Serikali ya Awamu ya Sita tutaanza kufanya miradi wenyewe, halafu mashirika yatatukuta njiani kisha tutakwenda nao. Tutaanza kwa fedha za ndani, kisha wakimaliza taratibu zao watatukuta tukiendelea,” amesema.

Aidha, amesema hali iliyotokea nchini wakati wa uchaguzi mkuu imeitia doa nchi, na kwamba huenda ikapunguza sifa ya kupata mikopo kirahisi, hivyo ameagiza viongozi kutafuta zaidi fedha za ndani ili kutekeleza miradi.

Send this to a friend