Rais Samia: Tutaendelea kuimarisha ushirikiano na China katika maendeleo ya kiuchumi

0
76

Rais Samia Suluhu Hassan amesema ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika umeleta matokeo chanya kwa maisha ya watu wa Afrika, hasa kupitia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na nchi hiyo.

Ameyasema hayo wakati akihutubia viongozi mbalimbali kwenye Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika katika ukumbi wa The Great Hall of the People Jijini Beijing nchini China ambapo katika hotuba yake, amesisitiza Tanzania kuimarisha ushirikiano wake na China, hasa katika miundombinu na maendeleo ya kiuchumi.

“Matokeo ya ushirikiano huu [China na nchi za Afrika] zinaonekana katika uchumi wetu, na ni kweli kwamba China imekuwa mshirika wa kweli katika mapambano yetu dhidi ya umasikini na katika kufuata ustawi,” amesema.

Aidha, Rais Samia amepongeza juhudi za China za kutimiza ahadi zilizotolewa wakati wa Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa FOCAC, hasa utekelezaji wa programu 9 zilizokubaliwa ambazo zimeleta maendeleo kwa mataifa ya Afrika licha ya changamoto za kiuchumi zilizotokana na janga la COVID-19.

Send this to a friend