Rais Samia: Tutafanyia kazi Ripoti ya CAG, TAKUKURU

0
10

Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali iko tayari kuendelea kufanyia kazi maoni na mapendekezo yaliyotolewa ndani ya taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG).

Aameyasema hayo wakati akipokea taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi ya TAKUKURU kutoka kwa Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Crispin Chalamila, pamoja na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere Ikulu jijini Dar es Salaam.

Katika hotuba yake, Rais Samia ameeleza kuwa ukaguzi uliofanywa na CAG unatoa taswira ya matokeo ya hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuziimarisha taasisi za umma nchini ili ziweze kutumia vizuri rasilimali za serikali, lakini pia ziweze kufuata taratibu zinazotumiwa katika matumizi ya rasilimali hizo.

Aidha, Rais Samia omeongeza kuwa licha ya mapungufu yaliyotajwa katika ripoti hiyo, ni faraja kuona kuwa kumekuwa na ongezeko la ufanisi katika matumizi ya rasilimali za Serikali.

Send this to a friend