Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali kushindwa kutoa huduma za msingi kwa wananchi kumechochea kuibuka kwa migogoro katika baadhi ya nchi za Afrika na kupelekea kuundwa kwa mifumo inayolenga kudhoofisha mamlaka za Serikali ambayo inaeneza matakwa ya wananchi kwa njia isiyofaa.
Ameyasema hayo leo katika ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Demokrasia ambao unawahusisha viongozi wakuu wastaafu wa nchi mbalimbali Afrika uliofanyika jijini Arusha.
“Mifumo hiyo ni kama na maandamano, wanaharakati, vikundi vya vurugu [..] haya yote yametokana na kutokutoa huduma muhimu za kijamii, na hapa ndipo baadhi ya vipengele vya demokrasia kama vile uhuru wa kujumuika na uhuru wa kujieleza vinapotumika vibaya,” amesema.
Aidha, amesema Serikali ina lengo la kujenga uchumi stahimilivu kupitia vijana, ambao utasimama kidete kupambana na mdororo wa uchumi na majanga mengine ya asili kama vile athari za mabadiliko ya hali ya hewa.
Mfahamu Rais mdogo mwanamke anayetarajiwa kufanya ziara Tanzania
“Serikali inawekeza katika maendeleo ya mtaji wa binadamu kupitia utoaji wa ujuzi wa kujifunza na kutengeneza ajira. Pia tunaimarisha uwekezaji katika miundombinu ya kilimo, utalii, uchimbaji madini na uchumi wa bahari, na sekta zingine ambazo zinaweza kutoa fursa nyingi za ajira kwa vijana.
Akizungumza kuhusu sera ya maridhiano nchini, amesema Tanzania imeweza kuimarisha umoja na kulinda amani na utulivu pamoja na kuondoa tofauti zilizopo kupitia majadiliano ambayo yamezaa matunda.