Rais Samia: Vijana wengi wamekosa lishe bora

0
41

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kutokana na matatizo yanayowapata vijana wengi na kushindwa kuzaa watoto wenye afya njema, chanzo kikuu ni kukosa lishe bora.

Ameyasema hayo katika hafla ya utiaji saini mkataba wa usimamiaji wa shughuli za lishe jijini Dodoma na kuwaagiza watafiti wa lishe kutafuta suluhu ili kuokoa kizazi kilichopo na cha baadaye pamoja na taifa kwa ujumla.

Rais Samia: Haki itapunguza mlundikano wa mahabusu gerezani

“Tukiacha hali iende hivi, tunakwenda kuwa na taifa goigoi [dhaifu], tunaenda kuwa na taifa lenye watu lakini si rasilimali watu, ni watu ambao ni mzigo kwa taifa si watu ambao watazalisha kwa ajili ya taifa, kuzalisha mali, kusimamia uchumi lakini pia kuzalisha wenzao ili taifa liendelee,” amesema.

Aidha, Rais Samia ameiagiza Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kuhakikisha watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi wanatambulika na Serikali na kusaidiwa ili kuepusha kuwa na taifa lenye vijana waharifu.

Send this to a friend