Rais Samia, viongozi wa CCM kuhudhuria uapisho wa Rais wa Zambia

0
34



Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ataondoka nchini kesho Agosti 24, 2021  kuelekea nchini Zambia kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Zambia, Hakainde Hichilema.


Sherehe  za Uapisho wa Rais huyo Mteule wa 7 wa Zambia zitafanyika katika Uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium), Jijini Lusaka.


Katika msafara wake Rais Samia ataongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Idara ya Oganaizesheni wa CCM, Maudline Cyrus Castico, Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mizengo Peter Pinda, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mzee Kombo Hassan Juma, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Henry Daffa Shekifu, na Mbunge wa Jimbo la Mtera na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Livingstone Joseph Lusinde.


Aidha, Rais mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atashiriki katika sherehe hizo akiwa Kiongozi wa timu ya Waangalizi wa Uchaguzi kutoka  Jumuiya ya Madola.


Send this to a friend