Rais Samia: Viongozi wa dini fundisheni vijana maadili

0
25

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa viongozi wa dini zote nchini kuongeza jitihada za kufundisha maadili, hususan kwa vijana.

Ameyasema hayo wakati akishiriki Kongamano la Wanawake wa Kiislam Zanzibar, ambapo amesisitiza umuhimu wa kuwatii na kuwaheshimu viongozi pamoja na viongozi kuwa waadilifu na weledi kwa watu.

“Watu waliopitishwa kwenye mafunzo ya dini hawezi kusimama akanyanyua mdomo akamtusi au akamkashifu kiongozi wake, kwahiyo wale wanaofanya ni kwa sababu hawakupita kwenye malezi ya kidini. Na wito wangu, huwa nasema na viongozi wa dini zote kukaa na kufundisha vijana wetu,” ameeleza.

Aidha, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa wananchi kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi na kuacha tabia za ukwepaji kodi, huku akieleza kuwa kwa Tanzania bara mapato yatokanayo na kodi yamepanda kufikia TZS trilioni 27.63 mwaka wa Fedha 2023/24 kutoka TZS trilioni 24.1 mwaka wa Fedha 2022/23.

Mbali na hayo, Rais Samia amesema Serikali haitavumilia vitendo vya upigaji ramli chonganishi zinazofanywa na baadhi ya watoa tiba za asili kwani zinapelekea mitafaruku kwenye jamii, na kwamba upigaji ramli chonganishi ni sehemu ya imani potofu na dhuluma inayopaswa kukemewa kwa nguvu zote.

Send this to a friend