Rais Samia: Wafanyakazi wana mchango mkubwa kukua kwa uchumi wa Tanzania 

0
36

Kufuatia pongezi zilizotolewa na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF) kuipongeza Tanzania kwa kukua kwa uchumi pamoja na mipango mizuri ya fedha, Rais Samia Suluhu Hassan amesema wafanyakazi wamekuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania.

“Wafanyakazi tunawathamini sana na tunawapongeza. Tuendelee kujituma taifa letu lizidi kukua,” amesema

Rais Samia ameyasema hayo katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ambayo kitaifa yalifanyika hapo jana mkoani Morogoro na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.

Aidha, amevishukuru vyama vya wafanyakazi na Watanzania kwa ujumla kwa kuona na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu sita pamoja na kutekeleza yale yaliyoahidiwa.

“Ninashukuru kwamba nilipokea shukrani na pongezi nyingi kutoka kwenu, kwa niaba yenu TUCTA wametoa shukrani kwa yale yote ambayo Serikali imetekeleza, yale ambayo tulikubaliana mwaka jana ambayo tumeyatekeleza tayari na yale ambayo yamo katika hatua mbalimbali za utekelezaji,” amesema.

Ameongeza kuwa “Nashukuru sana TUCTA mara hii wamenielewa [..] mara hii wamekuwa wapole, wamesema ‘mama baada ya uliyoyafanya kwa kweli uchumi wetu hauwezi tena.’”

Send this to a friend