Rais Samia: Wanasheria iangalieni kwa uzito DRC

0
39

Rais Samia Suluhu Hassan ameikiagiza Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki (EALS) kuiangalia kwa upana nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo kwa sasa ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hasa katika changamoto waliyonayo ya kiusalama inayowakabili.

Ameyasema hayao leo Novemba 24 alipokuwa akizungumza na wanasheria katika ufunguzi wa mkutano wa 27 wa Jumuiya ya Wanasheria wa Afrika Mashariki jijini Arusha, ambapo amekitaka chama hicho kuzingatia mfumo wa nchi hiyo kihistoria, kisheria, kiutamaduni, changamoto na fursa walizonazo.

“Kwa kuwa DRC sasa ni mwanachama wa ‘East African Comunity’, nataka chama chenu kiiangalie DRC [..] na muhimu zaidi sisi kama wana-Afrika Mashariki hatuna budi kutafakari kwa umakini kuhusu mustakabali wa ndugu zetu wa DRC, wanachangamoto nyingi, hali ya usalama upande huu wa mashariki si nzuri sana [..] wote tuna changamoto za kiusalama lakini si kubwa kama za wenzetu DRC,” amesema.

Aidha, amesisitiza kuzingatia misingi mikuu ya ibara ya 6 iliyoanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuzingatia misingi ya kidemokrasia, utawala wa sheria, uwajibikaji na uwazi huku akiwataka wanasheria kutenda haki na kukemea suala la rushwa kwa kuwatia hatiani raia wasio na hatia na kuwaacha huru ambao walistahili kutumikia vifungo magerezani.

Rais Samia: Wanasiasa wanachochea migogoro ili wapate kura za wananchi

“Sisi sote tunao wajibu wa kukuza utawala bora na kutetea haki za binadamu, na sijawahi kuona taifa lililoweza kufikia mageuzi ya kweli ya kijamii na kiuchumi kwa kukiuka utawala bora na utawala wa kisheria,” amesisitiza.

Ameongeza, “Mnapochukua rushwa kumtia mtu hatiani ambaye hana hatia na mwenye hatia mkamuacha huru, yule mwenye hatia anakwenda kuendeleza ubabe na kuvunja sheria akijua pesa yake itambeba, na yule ambaye hana hela anaishia jela na kumbe hakuwa wa kwenda huko.”

Send this to a friend