Rais Samia: Wanasiasa wanachochea migogoro ili wapate kura za wananchi

0
36

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wanasiasa kuacha kuchochea migogoro ya ardhi kwa wananchi kwa ajili ya manufaa yao binafsi badala yake wawaambie ukweli pindi wananchi wanapovamia maeneo yasiyo rasmi.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Manyara katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Kwaraa Novemba 23, 2022.

“Wakati wananchi wanavamia maeneo, wanasiasa hatuwaambii wananchi ukweli, tunawaangalia wakivamia na badala yake tunakuja kusimama kutetea wavamizi wa maeneo yale [..] lengo ni kupata kura huko baadaye wasikuone wewe ni mbaya,” amesema.

CHADEMA yatishia kutoshiriki uchaguzi mkuu 2025

Aidha, katika hotuba yake amewataka wananchi kuongeza jitihada kwenye kilimo ili miaka ijayo Tanzania isiwe miongoni mwa nchi zitakazokumbwa na balaa la njaa ambalo dunia inaweza kukumbwa.

Kutokana na hayo, Rais Samia ameeleza kuwa Tanzania imechukua hatua zote za kujikinga na janga hilo ikiwemo kuweka miundombinu ya kuzalisha mbengu, kujenga miundombinu ya kumwagilia, kilimo cha mashamba makubwa ili kupata chakula kingi na kuweza kuwauzia majirani.

Mbali na hayo, ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali pale ambapo kunatakiwa michango kutoka kwa wananchi waweze kuchangia ili kuiwezesha Serikalli kufanya miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kujenga mabwabwa ya kuhifadhi maji.

Send this to a friend