Rais Samia ziarani Ufaransa na Ubelgiji

0
44

Rais Samia Suluhu Hassan ameondoka nchini leo jioni ya leo kuelekea Ufaransa na baadaye Ubelgiji kwa ajili ya ziara ya kikazi katika nchi hizo.

Akiwa nchini Ufaransa, Rais Samia anatarajia kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari duniani.

Pia, atashuhudia utiaji saini baina ya Serikali ya Tanzania na Ufaransa katika sekta za miradi ya maendeleo, ushirikiano katika masuala ya uchumi wa buluu, usalama wa bahari, sekta ya usafiri na maendeleo endelevu.

Katika hatua nyingine Rais anatarajiwa kuzungumza na Watanzania wanaoishi nchini Ufaransa.

Send this to a friend