Rais Samia:Tanzania haijaathirika na mabadiliko ya tabia ya nchi kama nchi nyingine

0
13

Rais  Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania haijaathirika kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya tabia nchi yanayoikumba dunia, ikilinganishwa na mataifa mengine kufuatia kuwepo kwa mipango mbalimbali ya kukabiliana na athari za mazingira nchini.

Rais amesema hilo akijibu swali la waandishi wa habari kuhusu jijini New York, Marekani ambako pamona na  kuhudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais atahudhuria mikutano mbalimbali itakayojali masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Alipowasili jijini humo Mara amepokelewa na Watanzania wanaoishi nchini humo na kuwashukuru kwa mapokezi makubwa waliyomuonesha.

Send this to a friend