Rais Samia:Tuendelee kudumisha amani yetu kwa mustakabali wa taifa

0
44

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania inaendelea kutekeleza lengo la kudumisha amani na umoja hivyo Watanzania waendelee kudumisha tunu hiyo kwa mustakabali mzuri wa taifa.

Ameyasema hayo leo wakati akishiriki katika Maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na mchakato wa ukusanyaji maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma.

“Miaka 62 ya uhuru wetu imekuwa ni ya mafanikio kwa kiasi kikubwa. Pamoja na amani na utulivu, nchi yetu imepata maendeleo makubwa kwenye kila sekta, ziwe za kijamii au za kiuchumi,” amesema.

Aidha, amesema Serikali inaendelea kupambana na athari za ongezeko la bei ya mafuta duniani iliyochangiwa na vita vya Ukraine na janga la UVIKO-19, pamoja na uhaba wa dola za kimarekani, fedha inayotegemewa zaidi duniani.

Katika hotuba yake, Rais Samia ameeleza kuwa Tanzania imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kutekeleza lengo la kusomesha watoto bure katika elimu ya msingi, ambapo sasa Tanzania inatoa elimu bure hadi kidato cha Nne.

Send this to a friend