Rais Trump adai Rais wa Ukraine ni dikteta

0
11

Rais wa Marekani, Donald Trump amemuita Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky dikteta na kumuonya kuwa lazima achukue hatua haraka ili kupata amani, la sivyo anaweza kupoteza nchi yake.

Kauli hiyo imeongeza mvutano kati ya viongozi hao wawili na kuzua wasiwasi kwa viongozi wa Ulaya ambao wanahofia kuwa mtazamo wa Trump kuhusu kumaliza vita kati ya Russia na Ukraine unaweza kuisaidia Urusi.

Trump amedai kuwa Zelensky anafanya kazi mbaya naa kwamba amekuwa akinufaika na msaada wa kifedha na kijeshi wa Marekani akiwa na nia ya kurefusha vita na Urusi badala ya kutafuta suluhu.

Kauli hiyo imetolewa siku moja baada ya Trump kudai kuwa Ukraine ndio iliyoanzisha uvamizi nchini Urusi mwaka 2022.