Rais Trump afikishwa mahakamani, akana mashitaka yote

0
34

Rais Mstaafu wa Marekani, Donald Trump amefikishwa katika mahakama ya  jinai ya Manhattan kujibu mashitaka yanayomkabili .

Trump amekuwa Rais wa kwanza wa Marekani kukabiliwa na mashitaka ya uhalifu ambapo anakabiliwa na makosa 34 ambayo yanabeba kifungo cha juu cha miaka 136 na amekiri kutokuwa na hatia kwa makosa yote.

Mwandishi wa habari wa Marekani akamatwa Urusi kwa madai ya ujasusi

Mashitaka yanayomkabili ni pamoja na kudanganya juu ya biashara zake na kukusudia kuvuruga uchaguzi wa mwaka 2016.

Mawakili wake wamesema watapambana ili mashitaka dhidi ya Rais huyo yafutwe.

Hata hivyo, Trump hajatoa maoni yoyote kutoka kwa waandishi wa habari na anatarajiwa  kurejea nyumbani kwake Florida, ambako atazungumza hapo baadaye.

Send this to a friend