Rais Tshisekedi kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa

0
3

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Félix Tshisekedi ametangaza mpango wa kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kufanya mabadiliko katika uongozi wa muungano huo, wakati mashambulizi ya waasi wa M23 yakiendelea nchini humo.

Kauli hiyo imefuatia wakati serikali yake ikikabiliwa na shinikizo la kimataifa kuhusu kutafuta suluhisho la mgogoro huo mashariki mwa DRC.

Kutekwa kwa maeneo makubwa ya mashariki mwa Congo na waasi wa M23 kumeongeza hofu ya kuzuka kwa vita vikubwa zaidi na kumechochea baadhi ya wanachama wa upinzani uliogawanyika kutabiri hadharani kuwa urais wake hautadumu.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, DRC imepata hasara mfululizo katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, hali iliyochochea ukosoaji dhidi ya mkakati wa kijeshi wa serikali.

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC amesema Ijumaa kuwa waasi katika Jimbo la Kivu Kaskazini wanakwamisha operesheni za kulinda amani.

Send this to a friend