Rais: Viongozi mnaowalangua wakulima kwenye mpunga hamtendi haki

0
110

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wanaofanya biashara ya ununuzi wa mpunga kwa kuwalangua wakulima kuacha tabia hiyo kwani hawawatendei haki wakulima.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Ifakara mkoani Morogoro ambapo katika hotuba hiyo ameagiza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kununua mpunga wa mkoa huo kwa bei ya shilingi 900 kwa kilo badala ya shilingi 570.

‘’Viongozi mnapojiingiza kwenye biashara hii na kwenda kunyonya nguvu ya mkulima hufanyi haki. Uwe diwani, uwe sijui mwenyekiti wa nini, uwe ngazi yoyote, kama unafanya biashara hii ya kuongeza kipimo kwenye magunia ya mkulima na ukalipa kidogo ili wewe unufaike hufanyi haki, mkulima anapoteza nguvu yake kubwa, apate kwa jasho lake,’’ amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amewasihi wananchi katika maeneo mbalimbali nchini kutoanzisha makazi kwenye maeneo ya hifadhi na kuwaagiza viongozi na Serikali kulinda maeneo hayo ili kuepusha mizozo inayoweza kutokea baina ya wananchi na serikali.