Rais wa FIFA aipongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu

0
42

Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Gianni Infantino ameipongeza klabu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2022/23.

Katika salamu zake za pongezi alizoandika kupitia kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Wallace Karia amesema siyo rahisi kutwaa ubingwa huo pasipo bidii ya timu nzima, ari na kujitolea.

Rais Samia apandisha dau hadi milioni 20 kwa kila goli kwa Yanga

Infantino ametoa pongezi kwa wote waliohusika katika kufanikisha klabu hiyo kufikia mafanikio hayo akiongeza kuwa kila mmoja anaweza kujivunia kwa hilo.

Aidha, ameipongeza TFF kwa mchango wake katika maendeleo na ustawi wa soka la Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Send this to a friend