Rais wa Ivory Coast ashinda uchaguzi kwa asilimia 94

0
27

Tume ya uchaguzi nchinj Ivory Coast imemtangaza Rais Alassane Ouattara kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili baada ya kupata asilimia 94 ya kura zote.

Idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo uliosuswa na vyama vya upinzani ilikuwa takribani asilimia 54 ya watu wote waliojiandikisha.

Hata hivyo ushindi huo wa Rais Ouattara kwa muhula wa tatu unasubiri kuthibitishwa na Baraza la Katiba nchini humo.

Rais huyo aligombea kwa muhula wa tatu baada ya mgombea aliyekuwa ameteuliwa na chama tawala kufariki ghafla Julai mwaka huu.

Aidha, upinzani nchini humo umesema kuwa unaunda serikali ya mpito na itaandaa uchaguzi mpya baada ya kugomoea uchaguzi uliofanyika kutokana na Rais kugombea muhula wa tatu.

Uchaguzi huo ambao umegubikwa na vurugu umepelekea vifo vya watu 30 hadi sasa.

Send this to a friend