![](https://swahilitimes.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/Liberian-President-Joseph-Boakai.webp)
Rais wa Liberia, Joseph Boakai amewasimamisha kazi zaidi ya maafisa 450 wa serikali akiwemo waziri anayesimamia bajeti pamoja na mabalozi, kwa kushindwa kutangaza mali zao ndani ya muda uliowekwa.
Uamuzi huo unafuatia agizo la Rais lililotolewa Novemba 27, 2024, ambalo lilitoa muda wa nyongeza wa siku kumi kwa maafisa hao kutekeleza agizo hilo.
Maafisa hao wamesimamishwa kazi kwa muda wa mwezi mmoja bila mshahara au hadi watakapowasilisha tamko la mali zao kama inavyotakiwa.
Aidha, Rais Boakai ameonya kuwa kushindwa kutekeleza wajibu wa kutangaza mali kunahujumu juhudi za kitaifa za kupambana na ufisadi na kuhakikisha uwajibikaji.
Sheria ya Liberia inawataka watumishi wa umma kutangaza mali zao wanapoanza na wanapoacha nyadhifa zao.