Serikali ya Malawi itaokoa TZS milioni 608.13 kutokana na kufutwa kwa safari mbili za Rais Lazarus Chakwera kama sehemu ya hatua za serikali za kubana matumizi.
Rais Lazarus hatahudhuria mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola mjini Kigali, Rwanda, na Kongamano la Maendeleo ya Mfuko wa Opec huko Vienna, Austria, badala yake atawakilishwa na mawaziri.
Waziri wa Fedha, Sosten Gwengwe amewaambia waandishi wa habari kuwa serikali haijapiga marufuku safari za nje isipokuwa zile zisizokuwa na ulazima.
“Safari nyingine haziwezi kuepukika, kwa mfano Rais anakabidhi uenyekiti wa SADC kwa DRC mnamo Agosti, hiyo ni safari ambayo haiwezi kuwakilishwa,” amesema.
Malawi mwezi uliopita ilitangaza kushuka kwa thamani ya 25% ya fedha yake, Kwacha, kama sehemu ya marekebisho ya kupata ufadhili kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).