Rais wa Malawi avunja Baraza la Mawaziri, mawaziri watatu wapandishwa kizimbani

0
67

Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera amevunja baraza la mawaziri kutokana na kushamiri kwa vitendo vya rushwa.

Akihutubia Taifa Januari 24 mwaka huu Rais alisema kwamba atapambana na vitendo vyote vya ukiukwaji wa sheia nchini humo.

Mawaziri watatu kati ya hao wanakabiliwa na kesi za rushwa akiwemo waziri wa ardhi aliyekamatwa mwezi uliopita.

Waziri huyo anatuhumiwa kuchepusha fedha za UVIKO19, na waziri wa nishati kwa kupindisha mikataba ya mafuta kwa manufaa yake. Hata hivyo wote wamekanusha tuhuma hizo.

Chakwera alichaguliwa mwaka 2020 ahadi yake kubwa ikiwa ni kupambana na rushwa.

Send this to a friend