Rais wa Malawi awataka wananchi kutotegemea maendeleo kutoka kwa wanasiasa

0
36

Rais wa Malawi, Lazarius Chakwera amemtaka kila mwananchi kuwajibika katika maendeleo ya nchi kuliko kukaa na kila mara kutegemea wanasiasia kuwatimizia mahitaji yao.

Rais Chakwera amesema kuwa kwenye simu yake ana mamia ya jumbe kutoka kwa wananchi wanaoomba msaada wa kimaisha, kwa vile tu wanamuona yeye ni Rais, na kuongeza kwamba wabunge nao wana jumbe sawa kutoka kwa wananchi kwenye majimbo yao.

“Lazima tujidhibiti wenyewe dhidi ya tabia ya kuwaomba wanasiasa kutusaidia kuliko tunavyojifanyia wenyewe. Nchi yetu haitoendelea kwa mwendo huu,” amesema Chakwera.

Aidha, amewataka wananchi katika ngazi ya familia kutekeleza mipango inayokwenda sambamba na mipango ya Taifa ambayo anaizindua.

Amesisitiza kwamba haitojalisha ni mwanasiasa gani umemchagua kuongoza, au ni mara ngapi umemwambia mwansiasa huyo abadilike, endapo watu hawatobadilika.

Hapa chini ni video ya hotuba yake:

 

Send this to a friend