Rais wa Mali aliyepinduliwa alazwa hospitali

0
12

Rais wa Mali aliyepinduliwa hivi karibuni, Ibrahim Keïta amelazwa hospitali katika Mji Mkuu wa nchi hiyo, Bamako.

Hata hivyo bado hali ya kiongozi huyo haijawekwa wazi na bado haifahamiki tatizo linalomsumbua.

Kiongozi huyo mwenye miaka 75 alishikiliwa kwa siku 10 na jeshi la nchi hiyo, kisha akatangaza kujiuzulu nafasi hiyo akaachiwa kurejea nyumbani kwake.

Keïta aliripotiwa kuwaambiwa wasuluhishi wa mgogoro nchini humo kuwa hana nia ya kuendelea kuiobgoza nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Kabla ya mapinduzi yake, upinzani ulikuwa ukimtaka ajiuzulu kwa madai kuwa ameshindwa kusimamia uchumi wa nchi hiyo, kukithiri kwa rushwa na kushindwa kuthibiti mapigano ya waasi.

Send this to a friend