Rais wa Mali atangaza kujiuzulu baada ya mapinduzi ya kijeshi

0
42

Rais wa Mali ametangaza kuwa kujjiuzulu nafasi hiyo kuepusha umwagaji damu saa kadhaa baada ya kuwekwa kuzuizini na jeshi la nchi hiyo katika mapinduzi ya ghafla yaliyotokana na mgogoro wa kisiasa uliodumu kwa miezi kadhaa katika Taifa hilo la Afrika Magharibi.

Licha ya taarifa hiyo iliyorushwa na Kituo cha Televisheni cha Mali, bado haijafahamika kama sasa ni rasmi jeshi ndilo linaloongoza nchi hiyo.

Jumanne mchana wanajeshi waasi wa nchi hiyo walimkamata Rais Ibrahim Keita na Waziri Mkuu Boubou Cissé na kuwapeleka katika kambi ya jeshi iliyopo Mji Mkuu, Bamako ambayo waliiteka asubuhi kabla ya tukio hilo.

Wapinzani wameandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo wakionesha kuliunga mkono jeshi la nchi hiyo na kushinikiza Rais Keita kung’atuka madarakani.

Jumuiya za kimataifa pamoja na taasisi mbalimbali za Afrika zimekemea vikali tukio la kutekwa kwa viongozi hao, na kusema hawatounga mkono jitihada zozote za kukiuka katiba ya nchi.

Kw amuda mrefu kumeripotiwa kuwapo mgogoro na jeshi hilo uliochochewa na suala la malipo, vita dhidi ya magaidi pamoja na kutoridhishwa na utendaji wa Rais Keita.

Send this to a friend