Rais wa Uganda, Yoweri Museveni abadili jina lake

0
73

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amebadili jina lake ambapo sasa amejumuisha jina alilokuwa akilitumia utotoni, Tibuhaburwa.

Rais Mueveni alisaini hati ya kubadili jina hilo kama ambavyo inatakiwa na sheria ya usajili wa watu (Registration of Person Act), ambapo sasa atatambulika rasmi kama Yoweri Tibuhaburwa Kaguta Museveni.

Licha ya kuwa jina hilo limekuwa likitumika katika miaka yake 34 ya kuiingoza Uganda, halijawahi kutumika kwa umma.

Kwa mujibu kwa hati ya kubadili jina (deed poll) ya Oktoba 6, Museveni amesema kuwa alizaliwa Septemba 1944 na kupewa jina Yoweri Tibuhaburwa Kaguta. Hata hivyo vyeti vyake vya taaluma vina jina Yoweri Tibuhaburwa Museveni.

“Tangu kuhitimu elimu yangu, majina Yoweri Museveni, Yoweri Tibuhaburwa Museveni, Yoweri Kaguta Museveni na Yoweri Tibuhaburwa Kaguta Museveni yamekuwa yakitumika kunitambulisha mimi,” ameeleza Museveni kwenye hati yake ya kiapo.

Inaaminika kuwa hatua hiyo ya Rais Museveni imetokana na hitaji la tume ya uchaguzi nchini humo ambayo inataka jina la mgombea kwenye nyaraka za uteuzi lifanane na jina lililopo kwenye vyeti vyake vya kitaaluma.

Tume hiyo imesema kuwa watia nia ambao majina ya vyeti vyao vya taaluma yatatofautiana na majina ya kwenye nyaraka za uchaguzi hawatoteuliwa.

Send this to a friend