Rais wa Ujerumani kufanya ziara ya siku tatu Tanzania

0
13

Rais wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier anatarajiwa kufanya ziara ya siku tatu nchini kuanzia Oktoba 30, mwaka huu kwa mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Ziara hiyo imelenga kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kwa kuzingatia biashara na uwekezaji zikiwa kama nchi zinazofanya kazi pamoja katika sekta mbalimbali na maeneo yenye maslahi ya pamoja.

Rais Steinmeier atakutana na kuzungumza na mwenyeji wake, Rais Samia Suluhu, pia ataambatana na ujumbe wa viongozi wa wafanyabiashara kutoka makampuni makubwa ya Ujerumani ambao watashiriki katika Jukwaa la Biashara la Tanzania na Ujerumani Oktoba 31, 2023.

Rais Steinmeier pia anatarajiwa kutembelea makumbusho ya vita vya Maji Maji mjini Songea, na kuzungumza na familia ya wahanga wa vita hivyo.

Send this to a friend