Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu afariki dunia

0
54

Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73 Abu Dhabi imethibitisha.

Kutokana na kifo hicho serikali imetangaza siku 40, huku bendera kupeperushwa nusu mlingoti.

Pia, imetangaza sekta ya umma na sekta binafsi kusimamisha kazi kwa siku 3 kuanzia leo.

Sheikh Khalifa alizaliwa mwaka 1948 katika Mkoa wa Mashariki wa Abu Dhabi, kabla ya nafasi yake kama Rais, alikuwa mwanamfalme wa Abu Dhabi na aliongoza baraza kuu la petroli la Abu Dhabi ambalo linatayarisha sera ya mafuta.

Akiwa rais aliongoza moja ya hazina kubwa zaidi za uwekezaji duniani, huku sera zake za kisasa zikisaidia kubadilisha nchi yake kuwa nchi yenye nguvu ya kikanda.

Send this to a friend