
Mahakama nchini Peru imemhukumu Rais wa zamani Ollanta Humala na mkewe, Nadine Heredia, kifungo cha miaka 15 jela kwa makosa ya kutakatisha fedha.
Wanandoa hao walipatikana na hatia ya kupokea mamilioni ya dola kutoka kwa kampuni ya ujenzi ya Brazil, Odebrecht – pamoja na kutoka kwa serikali ya aliyekuwa Rais wa Venezuela, Hugo Chávez, ili kufadhili kampeni zao za uchaguzi wa mwaka 2006 na 2011.
Mara baada ya hukumu hiyo, Nadine Heredia aliomba hifadhi ya katika Ubalozi wa Brazil uliopo Lima, hatua iliyothibitishwa na mamlaka za Brazil.
Humala anakuwa Rais wa tatu wa Peru kufungwa kwa makosa ya rushwa ndani ya kipindi cha miaka 20 iliyopita.