Rais wa Zimbambwe awateua mwanae na mpwa wake kuwa Naibu Mawaziri

0
45

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amelaumiwa kwa upendeleo baada ya kumteua kijana wake wa kiume kuwa Naibu Waziri wa Fedha katika baraza jipya la mawaziri mara baada ya kushinda kiti cha urais awamu ya pili.

Siku ya Jumatatu alimteua mtoto wake, David Kudakwashe Mnangagwa na kumteua pia mpwa wake, Tongai Mnangagwa kuwa Naibu Waziri wa Utalii kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80 anakabiliwa na jukumu la kujenga upya uchumi uliokumbwa na ukosefu wa uwekezaji kutoka nje, ukosefu wa ajira, mfumuko wa bei na dola ya ndani ambayo imeporomoka kwa asilimia 80 mwaka huu.

Kuchaguliwa tena kwa Rais Mnangagwa mwezi uliopita kumepingwa na upinzani ukitaja madai ya udanganyifu, huku baadhi ya waangalizi wa uchaguzi wakisema kuwa uchaguzi huo huikukidhi viwango vya kikanda na kimataifa.

Send this to a friend