Rais Zuma aachana na mchumba wake mwenye miaka 25

0
36

Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma anadaiwa kuwa ameachana na mchumba wake mwenye miaka 25, Nonkasyiso Conco.

Taarifa kutoka nchini humo zinaeleza kuwa wawili hao waliachana mwaka jana na Conco amehama kutoka kwenye nyumba aliyokuwa amepangishiwa na Zuma jijini Durban.

Vyanzo vya karibu na wawili hao vinadai kuwa Conco aliambiwa afanye kuachana huko kuwe siri. Walinzi katika nyumba aliyokuwa akiishi mwanadada huyo wamesema kuwa alihama Disemba 2019, mara baada ya kutembelewa na Rais Zuma kwa mara ya mwisho.

Baba yake, Fartescue Cocnco, amethibitisha binti huyo kuhama na amesema sasa anaishi na mama yake.

Conco aligonga vichwa vya habari mapema mwaka huu kufuatia chapisho lake katika mtandao wa Instagram kutafsiriwa kuwa anamlea mwanae bila usaidizi wa baba.

Katika chapisho hilo aliandika kuwa malezi ya mtoto yanahitaji wazazi wote wawili, na inapotokea mzazi mmoja hayupo kutimiza majukumu yake, hali hiyo husababisha maumivu ya moyo.

Hata hivyo baadae alikanusha kuwa ameachana na mzazi mwenzake, kama ambavyo watu walivyotafsiri.

Send this to a friend