Ramadhan Brothers washika namba 5 America Got Talent

0
46

Wanasarakasi kutoka Tanzania, Ramadhani Brothers wameshika nafasi ya tano katika shindano maarufu duniani la kusaka vipaji la American Got Talent (AGT) lillofanyika nchini Marekani.

Kundi hilo limeonesha mitindo yao wa sarakasi ya kushangaza mbele ya majaji wanne akiwemo Simon Cowell, Sofia Vergara, Heidi Klum na Howie Mandel ambapo Adrian Stoica ndiye aliyeibuka mshindi.

Katika ukurasa wao wa Instagram, Ramadhani Brothers wameandika “Hatujapata kura za kutosha, tumekuwa watano katika shindano, na tunashukuru AGT kwa nafasi hii na watu wote waliotupigia kura, mapambano yanaendelea.”

Nyimbo 10 za Tanzania zinazotazamwa zaidi YouTube Agosti 2023

Ramadhan Brothers walifanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo Oktoba, 2022 baada ya mmoja wa waamuzi kubonyeza kitufe cha dhahabu (Golden Buzzer) kama ishara ya kuvutiwa sana na onesho la wasanii hao.

Send this to a friend