Ras Al Khaimah na Zanzibar zaongeza kasi ya ushirikiano wa kiuchumi baina yao

0
27

ABU DHABI — H.H. Sheikh Saud bin Saqr Al Qasimi, Mjumbe wa Baraza Kuu na Kiongozi wa Ras Al Khaimah, amempokea Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzubar, Dkt. Ali Mohamed Shein, kwa ajili ya mazungumzo ya masuala mabalimbali yenye maslahi baina ya pande mbili, na namna ya kukuza ushirikiano wa kibiashara, kiuchumi na kitalii.

H.H. Sheikh Saud amepongeza uwepo wa ushirikiano wa muda mrefu kati ya Falme za Kiarabu (UAE), hasa Ras Al Khaimah, na Zanzibar, huku akisisitiza kuimarishwa kwa ushirikiano huo na kukuza uwekezaji na biashara.

Kwa upande wake Dkt Shein, ameeleza shukrani zake kwa Sheikh Saudi huku akitanabaisha kuwa nchi yake iko tayari kuimairsha ushirikiano wa kimkakati na UAE.

Pia aliisifu Kampuni ya RAKGas Zanzibar Limited, akisema kuwa anaimani utafutaji na uchumbaji wa gesi unaofanywa na kampuni hiyo utatoa fursa za kiuchumi kwa Zanzibar na Ras AI Khaimah.

Ushirikiano wa karibu kati ya Ras AI Khaimah na Zanzibar umechagizwa na RAKGas Zanzibar Ltd kusaini makubaliano ya uzalishaji wa mafuta na gesi na Shirika la Maendeleo ya Petroli la Zanzibar (ZPDC) Oktoba 2018.

Makubaliano hayo yanaziwezesha pande hizo mbili kusimamia na kutekeleza shughuli za utafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta katika kitalu cha Pemba chenye ukubwa kwa kilomita za mraba 11,868.

Haya ni makubaliano ya kwanza ya aina yake ambayo Zanzibar imeingia tangu kuanza kutekelezwa kwa Sheria ya Mafuta na Gesi ya mwaka 2016 ambayo inaipa mamlaka juu ya bidhaa hizo.

H.H. Sheikh Mohammed bin Saud bin Saqr Al Qasimi, Mwana Mflame wa Ras Al Khaimah, alikuwepo wakati wa mazungumzo ya viongozi hao wawili katika jumba la kifalme lililopo katika Mji wa Saqr bin Mohammed, pamoja na ujumbe uliokwenda na Rais wa Zanzibar.

Send this to a friend