Msanii Raymond Mwakyusa, maarufu Rayvanny amewajia juu watu wanaosema kuwa amezidi kufanya ‘remix’ za nyimbo zinazofanya vizuri kutoka kwa wasanii wenzake nchini hususani wanaochipukia ili kuendelea kuvuma.
Hivi karibuni msanii huyo ameachia remix ya wimbo wa ‘Huu Mwaka’ wa msanii Dayoo ambao umezua mijadala mingi katika mitandao ya kijamii baada ya msanii huyo kutoka kufanya remix nyingine na msanii Miso Misondo.
Rayvanny amejibu kwa kuandika kuwa “ningetaka kufanya nyimbo zilizohit ningefanya ‘Enjoy’ [ya Jux na Diamond] ningefanya ‘Am single’ [ya Harmonize] tena hadi beat nilitumiwa na mzee Konde, so ukiona nimefanya wimbo basi nimeamua kufanya.
TFF: Hakuna fedha za maandalizi zilizotolewa na CAF kwa timu zilizofuzu AFCON
Msifanye nianze kukataa kufanya nyimbo na vijana wenzangu wakiomba tufanye kazi. Usichokijua ukiona nimefanya remix ya nje jua nimelipwa tena hela nyingi,” ameandika.
Hata hivyo, baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii wamemuunga mkono wakisema kwa kufanya hivyo kunamfanya asipotee kwenye muziki na kuwepo midomoni kwa watu kwakuwa yeye sio mtu wa ‘trends’ na wengine wakisema ni faida kwa wasanii wenye nyimbo hizo kwani zinawaongezea mashabiki.