Rayvanny: Nimekua kimuziki tangu niondoke WCB

0
30

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ amesema tangu aondoke kwenye lebo ya WCB amejihisi kukua kimuziki na kwa sasa anawaza mambo makubwa zaidi.

Akizungumza na HabariLeo, amesema changamoto anazokutana nazo pamoja na ushindani uliopo kwenye gemu ya bongo fleva, vimemkomaza zaidi.

“Ukweli sijutii maamuzi yangu, zaidi napambana ili niweze kuwa mkubwa zaidi, sababu huku kila kitu wakuulizwa ni mimi na sababu ndiyo bosi mkubwa ninayehusika na mambo yote ikiwemo kulipa wasanii na mengineyo,” amesema.

Tanzania Prisons na Singida Big Stars zafungiwa kusajili

Aidha, amesema kwa jinsi anavyofanya vizuri katika gemu hiyo, anaamini mpaka kufikia mwaka ujao atakuwa miongoni mwa wasanii wakubwa nchini na wenye wafuasi wengi kuliko ilivyo hivi sasa.

Send this to a friend