RC aagiza kukamatwa mwanahabari aliyesambaza video ya ‘shule’ chakavu

1
47

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali, Wilbert Ibuge ameagiza kukamatwa kwa mwandishi wa habari anayedaiwa kusambaza kipande cha video kwenye mtandao wa kijamii kuhusu madai ya uwepo wa Shule ya Msingi Litapatile katika Halmashauri ya Madaba, Wilaya ya Songwe Mkoani Ruvuma.

Agizo hilo lilitolewa baada ya video hiyo iliyosambaa  ikiwaonesha wanafunzi wamevalia sare za shule akidai kuwa wanasoma darasa la awali hadi darasa la tatu katika kibanda cha miti kilichoezekwa kwa nyasi.

Mkuu wa Mkoa huo amekanusha kuwepo kwa shule hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mkoani humo na kuwa eneo hilo linakaliwa na jamii ya wafugaji wakitokea Mtyangimbole waliokwenda kuishi porini wakitafuta malisho ya mifugo, hivyo huo ni uzushi wenye lengo la kuichafua Serikali.

“Huko hakuna miundombinu ya barabara ya kufika eneo hilo lililoko umbali kati ya kilometa 48 hadi 50 kutoka kijijini hapo, watoto hao wana haki ya kupata elimu kwa mujibu wa katiba na wazazi wana wajibu wa kuhakikisha wanaandikishwa na kuhudhuria masomo kwa mujibu na utaratibu,” amesema.

Amesisitiza kuwa, eneo hilo siyo makazi rasmi yanayotambulika kisheria na Serikali kupatiwa huduma za kijamii ikiwemo shule, hivyo kitendo kilichofanywa na wazazi hao hakikubaliki na kuamuru kukamatwa wazazi  waliothubutu kuwavalisha sare ili kuudhalilisha mkoa huo.

Send this to a friend